Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na
kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi
kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa
pamoja kwa kipindi chote cha maisha.
Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya
wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na
kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya
uzuri.
Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa
na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa.
Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na
umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa
nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa
kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu
kumtakiwa kwamba anataka kumuoa.
MWEYE MAPENZI YA KWELI
Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka
kwa mwanamke na ikiwezekana waweze kupata watotoa ambapo watoto mara
ndio wamekuwa furaha ya ndoa. Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi
kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga.
Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama
kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya
dhati kutoka moyoni mwake. Mwanamke asiye na mapenzi ya dhati utamgundua
tu, muda mwingi utamuona macho yake yako kwenye mfuko wa mwanaume.
Akiona kwamba mfuko umetuna utaona anaonesha mapenzi ya hali ya juu
lakini pindi hali inapokuwa kubwa mbaya kifedha mapenzi yanaanza
kufifia.
Kwanini wanaume wanapenda wana wake wenye mapenzi ya dhati kutoka
mioyoni mwao na si kutokana na fedha walizonazo? Hii inatokana na ukweli
kwamba maisha siku zote yanabadilika, kama waswahili wanavyosema, kuna
kupanda na kushuka.Sio kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama
itatokea hivyo basi ushukuru mungu.Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima
afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote
wa maisha yao na si kwa kipindi fulani tu cha neema.
Si hivyo tu pia asilimia kubwa ya maisha ya ndoa yanatawaliwa na
mapenzi, kwa hiyo nyanja hiyo inakuwa ya msingi sana kwa wanaume wengi
kuiangalia ili wasije wakajikuta wanaoa mwanamke ambaye baada ya muda
mapenzi yanakwenda likizo hali ambayo inaweza kuwafanya wasiishi maisha
ya raha mustarehe.
WENYE TABIA NZURI
Tabia njema ndio silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu
atakupenda, hiyo ni katika maisha ya kawaida. Lakini linapokuja suala na
kuoa tabia inakuwa kitu cha awali sana kungaliwa na hiyo inaweza kuwa
na ukweli kwa sababu wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na
maumbile mazuri, lakini wanakosa wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani
utaambiwa anatabia mbaya. Naweza kusema hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa
kwa baadhi ya wanawake kukosa wanaume wa kuwaona. Hakuna mwanaume hata
mmoja kati ya wale ambao nimejaribu kuongea naye ambaye ameonesha
kulidharau suala hilo la tabia.
Si hivyo tu wapo wanaume ambao wameingia kichwa kichwa na kuoa kwa
kuangalia sura tu bila kujali tabia, matokeo yake baada ya siku chache
yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo imepelekea kuvunjika kwa
ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo mwanamke.
WENYE UCHU NA MAENDELEO
Hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi
sasa hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani
'golikipa'. Kama atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa maendeleo kwa
kujituma kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kama vile kilimo kwa
wale walio vijijini na biashara ndogondogo kwa wale ambao wako mijijini
na hata vijijini. Ile dhana ya kusema mwanamke ni mama wa nyumbani wa
kukaa na kujipodoa akimsubiria mwnaume arudi amstarehesha, sasa hivi
imepitwa na wakati. Wanaume wengi wanapenda wanawake ambao ni
wahangaikaji, wenye ndoto za maendeleo katika maisha yao. Hata kama
watakuwa si wafanyakazi lakini wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao
juu ya jinsi gani wafanye ili wafanikiwe.
WASIOPENDA MAKUU
Kuna wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba
yaweza kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila
kujali hali halisi ilivyo. Kuna wanawake naweza kusema wana tamaa, kila
wikiendi utamsikia "leo tunakwenda wapi dear?" Akimuona rafiki yake
kanunua simu ya laki tatu na yeye utamsikia akisema, ‘na mimi naomba
uninunulie simu kama ya Grace’. Ukienda naye Pub anakuambia, "mimi
sinywi pombe za chupa natumia za kopo tena Heineken’. Yeye hajali kiasi
cha pesa mwanaume alicho nacho na usipotekelezea anachukia na anaweza
hata kupunguza mapenzi.
Wanawake kama hawa wako katika mazingira magumu sana ya kuweza kupata
wanaume wa kuwaoa. Mara nyingi katika maisha fedha huzungumza, kama
mwanaume atakuwa na pesa ya kutosha itakuwa rahisi sana kwa mwanamke
kupata kila atakachopenda lakini si kwa kumwambia mimi nataka kitu
fulani.Mwanaune mwenyewe utamsikia akisema, ‘unataka nikununulie simu ya
aina gani, au leo unataka twende wapi?’ hapo ndipo utakuwa na nafasi ya
kusema, ‘mimi nataka uninunulie simu kama ya fulani ama leo nataka
twende sehemu fulani.’
Wanaume ni warahisi sana wa kuwapatia wale ambao wanatarajia kuwaoa
chochote ambacho watahitaji kama tu pesa haitakuwa tatizo. Kitu ambacho
kinawaudhi wanaume wengi ni ile tabia ya mwanamke kupenda mambo makubwa
bila kuangalia uwezo uliopo kwa mwanume.
Kuna wanawake wengine wao si wasemaji kabisa, yeye anasubiri leo
amemletea hiki, anapokea na kushukuru, kesho akiambiwa twende beach
anakubali. Au wengine wanasubiri mpaka waulizwe wanataka nini, ndio
wanasema.
Sisemi kwamba uwe mkimya tu hata kama una shida ya kitu fulani na
unafahamu kwamba ukimweleza mwenza wako anaweza kukusaidia, hapana! kama
unaona kwamba uwezekano wa kupata kile ambacho unakihitaji upo mweleze
kwa utaratibu naamini atakuelewa na kukutimizia.Tabia ambayo hawaipendi
wanaume wengi ni ile ya kulazimisha ufanyiwe kitu fulani wakati
inawezekana uwezekano haupo.
WAVUMILIVU
Wapo wanawake ambao sio wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua kwamba
maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama
kifedha.Huu ndio wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke
anatarajia kwamba siku zote ni
Uvumilivu kwa mwanamke utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati
kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanamke mweye mapenzi ya dhati ni
lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina
yoyote, yawe ya raha ama ya starehe.Hawa ndio wale ambao wanaume wengi
wengependa kuwa nao maishani mwao.
Licha ya kupenda kuoa wanawake amabo wana tabia hizo nilizozitaja hapo
juu, wanachukizwa sana na wanawake ambao wanavijitabia vidogo vidogo
ambavyo kimsingi havikubaliki katka jamii.Tabia hizo ni kama wambea,
wasio wakweli na wawazi, wasioridhika, wagumu kusamehe na wapesi wa
kuchukia, wagomvi na wenye roho ya kwanini.
Utafiti huu umefanyikwa kwa baadhi ya wanaume ambao wanatarajia kuoa
wanawake ambao wanaoishi katika maeneo mbalimbali jijini Dar-es-Salaam.
Kwa maana hiyo basi hiyo iwe changamoto kwa wanawake. Wajue kwamba
wanaume wanafurahi kuwa na wanawake wa aina gani. Hata kama utakuwa
umeshaolewa, kama kuna wakati kunakuwa na kutokuelewana baina yenu,
chunguza yawezekana kwamba unakosa mojawapo ya tabia ambazo nimezitaja
hapo juu. Waweza kubadilika kwani inawezekana
ADS

tangazo kwa wasanii wanaopenda kutoka kimziki, usambaze mziki wako kwenye blog mbalimbali nchini ili uweze toka kimziki, je unataka kuutangaza mziki wako zaid ya nchi kumi kwa kuuweka kwenye blog mbalimbali kubwa TANZANIA wasiliana nasi wathsap 0768649181 au 0656475442
POST
Friday, 7 July 2017
Mabinti Siri Ishafichuka Wanaume Hupenda Wanawake Wenye Tabia Hizi
Diterbitkan July 07, 2017
Tags
Artikel Terkait
This Is The Oldest Page
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon